Friday, 18 May 2018

MAKONDA ATOA ONYO KALI KWA WANAWAKE

Na Shani Seif

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaonya wasichana wa mkoa wake wa Dar es salaam kutokubali kuolewa na wanaume wanaoishi katika maeneo ya bondeni ambayo ni hatarishi hasa katika kipindi cha mvua za masika.



Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam


Makonda amesema hayo alipofanya ziara katika eneo la mbagala kiburugwa na kuona baadhi ya nyumba za wananchi ambazo zimeathirika kutokana na kujengwa katika maeneo hatarishi na kuwataka wakazi hao kuhama mara moja.

Makonda ameongeza kuwa serikali  haitaweza kutoa msaada wa chakula na malazi kila mara kwa wananchi ambao wanakumbwa na majanga yanayotokana na wao kuamua kukaa katika maeneo hatarishi kwa kujitakia.




Baadhi ya wakazi wanaokaa mabondeni

Mkuu wa mkoa huyo amedai kuwa maeneo hayo ni ngumu kwa mwananchi kupata msaada wa dharura ikiwemo gari la wagonjwa au huduma ya zima moto.

Yanga kukupiga na rayno sport leo

Na Pamela chamafwa

Baaada ya kupokea kipigo kizito cha mabao 4-o dhidi ya kikosi cha sumlalyer ya nchi Algeria.








kikosi cha wana jangwani leo tarehe 
15/2/2018 wanachuana leo dimbani kukipiga dhidi ya kikosi cha rayor sport cha nchini Rwanda katika mchezo wa pili hatua ya makundi.

MAJALIWA ATOA AGIZO KUHUSU MAFUTA

Na. Pamela chamafwa
Dar es salaam.

Waziri mkuu wa jamhuri  ya muungano wa Tanzania mh.kassimu majaliwa amehitimisha mjadala wa kuwataka wafanyabiashara  wote hapo nchini kuingiza mafuta hayo sokoni ndani ya saa 72 .
Majaliwa ametoa agizo hilo baada ya spika wa bunge joh ndungai kuitaka serikali kueleza ufumbuzi wa tatizo la kuadimika kwa mafuta na kukwama kwa meli za mafuta bandarini kutokana na tatizo la kodi.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa


Kwa upande wake waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Charles mwaijage amesema mahitaji ya mafuta nchini ni kati ya tani laki 4 hadi 4 na nusu kwa mwaka huku vyanzo vya mafuta hapa nchini ikiwa ni asilimia 30 pekee.

WANAFUNZI WAJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA KUPIGA KURA

Na Shani Seif

Mchakato wa Uchaguzi   unafanyika siku hii ya leo katika chuo cha Uandishi wa habari cha TIME SCHOOL OF JOURNALISM TSJ . Wanafunzi chuoni humo wanafanya zoezi  la kupiga kura la kuchagua viongozi ngazi ya Urais na makamo wa urais.

Uchaguzi umesimamiwa kikamilifu na walimu ,mwenyekiti wa tume pamoja na viongozi ukizingatia usalama na utulivu wa wanafunzi kufanya zoezi hilo bila vurugu.


Mmoja wa wanafunzi akipiga kura
Wanafunzi wakijiandaaa kupiga kura

Chumba cha kupigia kura


Aidha wanafunzi wameonekana wakifanya zoezi hilo la kupiga kura kwa utulivu huku wakiwa na shauku kubwa ya kusubiri matokeo ambayo yanatolewa siku hii ya leo baada ya zoezi la kupiga kura kukamililka

WATU WAWILI WANUSURIKA KATIKA AJALI


Na Shani Seif

Ajali mbaya imetokea asubuhi  hii leo  majira ya saa moja  kaika  Barabara ya Al  Hassan mwinyi eneo la sayansi. Barabara hiyo ambayo ipo katika matengenezo  na bado haijakamilika




Polisi wakiwa wanachunguza ajali


   Wadada wawili wamejikuta gari lao Escudo likigeuka lilikotoka na kuwa miguu juu mbele kabisa la jengo la kituo cha sheria na haki za binadamu  na kupata majeruhi madogo madogo  na mmja wake kukimbizwa hospitali kwa kupata huduma ya kwanza



Gari aina ya Escudo likiwa limepinduka

Mmoja wa majeruhi (kushoto) alienusurika katika ajali hiyo




Thursday, 17 May 2018

IJUE KAULI MBIU YA SIKU YA MAMA 2018

NA AMINA SANGAWE


Siku ya kimataifa ya mama Duniani ilianzishwa rasmi mwaka 2009 na umoja wa mataifa nahuadhimishwa kila mwaka April 22 ili kutoa nafasi ya kuthamini umuhimu wa mama katika hii dunia.
Siku hii maalum kwa kina mama duniani huambatana na kauli mbiu ambayo kwa mwaka huu ni’’SITISHA UCHAFUZI WA MAZINGIRA PLASTIKI’’.kauli hii imetokana na waraka wa Baba mtakatifu Fransisko usemao’’Ujumbe huu ambao umesheheni  mapokeo ya kidini pamoja na ushauri wa kisayansi unaweza kufanyiwa kazi katika ngazi mbalimbali kuanzia kwa watu binfsi,vyama vya kiraia,serikali na mashirika ya kimataifa ili kukuza na kuimarisha mchakato wa maendeleo endelevu,usawa na kuzingatia haki za msingi kibinaadamu.
Siku ya mama duniani huadhimishwa nan chi nyingi ikiwemo Tanzania ,Lengo kuu la kuadhimisha hii siku ni kwaajili ya kumshukuru mama wa familia,pamoja na umama,uzazi wanaopitia pamoja na mchango wao mkubwa katika jamii


MASELE APANDA CHEO


NA AMINA SANGAWE.

Mbunge wa shinyanga mjini kwa tiketi ya CCM,Stephen Masele amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Bunge la  Afrika [PAP].

Taarifa hiyo imetolewa mei 11 mwaka huu Bungeni Mjini Dodoma  na mwenyekiti wa Bunge,Andrew Chenge na kubainisha kuwa mbunge huyo kijana amechaguliwa mei 10 mwaka huu.

Cheng amemsifu mbunge huyo kwa utendaji wake mzuri wa kazi na kuongea ‘’umelipa Bunge letu sifa na Tanzania kwa ujumla.Nafasi hii  ni ya kuitangaza nchi yetu na Bunge hili na tunamtakia kazi njema huko aendko.



UDART YISHTAKI SERIKALI


NA AMINA SANGAWE


Kampuni ya mradi wa usafirishaji ya mabasi ya mwendo kasi[UDART]imefungua kesi mahakamani dhidi ya serikali kupinga kitendo cha kuletwa mwekezaji mpya.

Hatua ya serikali kutafuta mwekezaji mwingine imetangazwa Mei 10 mwaka huu na Waziri  MkuuKasim Majaliwa akiwa Bungeni baada ya kampuni hiyo kuonekana kusuasua katika utendaji wa mradi huo.

Bila kusahau kampuni ya Udart imewahi kufunguliwa kesi ya madai mahakamani na kampuni ya Maxam wiki tatu zilizopita kwa kushindwa kulipa gharama za uendeshaji,uwekezaji na haki stahiki za wafanyakazi.


UCHAGUZI WATIKISA CHUO CHA UANDISHI TSJ

Na. Pamela chamafwa  
Dar es salaam .
Zoezi  la uchaguzi wa serikari  ya wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari  Tsj  limeendelea kuwa pasua kichwa baada ya kampeni  za wagombea kupamba moto

Wagombea watatu wana chuana vikali katika nafasi ya uraisi  na wagombea wa wili katika nafasi ya umakamu wa urais wanao shiriki katika nafasi ya Rais ni Kulwa Karedia Jacton, Abdulrahman Kinana, na Rashidi Rashidi huku nafasi ya makamu wa uraisi ikiwaniwa na  Aisha Charlse pamoja na Mohamed Ng’oula




Badhi ya wanafunzi  chuoni hapo akiwemo Richard Deo wamesema nivigumu kutabiri ni mgombea gani atakae weza kuibuka mshindi kutokana na kampeni zinazoendelea


Zoezi hilo la uchaguzi litahitimishwa may 18 ambapo wanafunzi wote watajumuika kupiga kura ili kuwachagua rais na makamu wa rais kama ilivyoanishwa na tume ya uchaguzi chini ya mwenyekiti odrian niclous  

NA :KHADIJA M HASSAN

  • MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI 

Hivi ndivyo hali ilivyokatika maeneo meng jijini dar es salaam kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha
kwa mujibu wa mamlaka ya ha li ya hewa imesema kua mvua zinazozidi milimeta 50 kwa saa 24 itaendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa pwani ikiwemo dar es salaam na visiwa vya unguja na pemba hali hiyu inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua
Hai ni kama ilivyo njia hazipitiki

baadhi ya nyumba za kinondoni kwa msisiri zikiwa zimezungukwa na maji kila pembe

UCHAGUZI WAPAMBA MOTO TSJ



              

Na Juliani Salvatory

    Uchaguzi wa serikali ya Wanafunzi Time School of Journalism umezidi kupamba moto hii ni baada ya wagombea wa nafasi ya Uraisi chuoni hapo kuendelea na shughuli za kampeni za kunadi sera zao kwa wanafunzi.

Uchaguzi huo unao talajiwa kufanyika siku ya ijumaa ya Tarehe 18-5-2018, unaonekana kuwa na maswal mengi kuhusu nani hatakayeibuka mshindi katika uchaguzi huo hii ni kutokana na wagombea kuwa na sera nzuri za kimaendeleo katika chuo hiko.
Habari Picha-

Mgombea wa nafasi ya Uraisi Rashid Hassan akizungumza na baadhi ya Wanafunzi mapema leo chuoni hapo.

Mgombea wa nafasi ya uraisi Rashid Hassan akiwa katika moja ya darasa chuo hapo akiendelea na shughuli za kampeni.

mgombea wa nafasi ya Uraisi Rashid Hassan katika,akiwana kampeni manager wake kushotoni Edwadi Benson wakati kulia ni Neema Edisoni.

Wednesday, 16 May 2018

MVUA ZAWA GUMZO JIJINI DAR ES SALAAM


           


  Na Juliani Kasimiri

  Mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Dar es salaam zimeonekana kuwa gumzo kubwa hii ni kutokana na mvua izo kunyesha mara kwa mara,nakupelekea athari kubwa kwa wakazi wa mkoa huo hususani wa maeneo ya mabondeni
Mvua hizo zinatakribani wiki moja tokea zianze kunyesha katika maeneo mengi mkoa humu,lakini zimeonekana kuwa na athari kubwa za kiuchumi na kimiundombinu.
Hussain Bakari ni mfanyabiashara katika soko la buguruni,kwa upande wake mvua hizo zimemfanya ashindwe kufanya biashara zake za kupanga mboga mboga hii ni kutokana na kunyesha mara kwa mara kwa mvua hizo.


Asha Mussa ni mkazi wa buguruni yeye anaona mvua hizo zimefanya usafiri kuwa mgumu hususani anapotaka maeneo yake ya kazi kuelekea nyumbani.

Ata ivyo watu mbali mbali katika mkoa huo wameonekana kuendelea na shughuli zao za kujipatia kipato,licha ya mvua hizo kuendelea kunyesha katika maeneo mengi jiji hapa. 

MASHIMO YAWA KELO KWA MADEREVA BARA BARANI


        
  Na Juliani Salvatory.

       Kuongezeka kwa mashimo katika Bara bara nyingi mkoani Dar es salaam kumeonekana kuwa ni kelo kubwa kwa madeleva watumiao bara bara hizo.
Licha ya Serikali kutumia gharama kubwa katika utengenezaji na ukarabati wa miundombinu hiyo ya bara bara,lakini bara bara hizo zimeonekana kuwa chini ya kiwango kinachopelekea kuwa na mashimo mengi katika jiji la Dar es salaam.
Sadam Jumanne ni dereva boda boda maeneo ya buguruni,kwa upande wake anaona mashimo hayo yamezidi kuwa mengi  na kuiomba serikali kuchukuwa hatua katika kukarabati miundombinu ya bara bara hizo.
Bakari Simi yeye ni dereva wa dala dala ziendazo Buguruni-Makumbusho,kwa upande wake anaiomba serikali kuchukua juhudi za haraka katika kukarabati mashimo hayo kwani upelekea ubovu wa vyombo vyao vya usafiri.
Wakandarasi wanaopewa tenda ya kutengeneza miundombinu ya bara bara wanapaswa kutengeza bara bara zenye ubora na zinazokidhi maitaji ya watumiaji wa bara bara hizo,kwani itasaidia kuepusha ajali mbali mbali zisizo na hulazima.  


IMG-20171016-WA0066

NA.PATSON MWITA.

MCHEZAJI wa timu ya Bombom Fc ya Ilala, Suleiman Mohammed anayefahamika kwa jina la Berko  anayecheza nafasi ya Golikipa namba moja wa timu hiyo,ambapo hadi sasa amedumu katika klabu hiyo kwa muda wa miaka tisa[9],alianza kupenda soka tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili[12],kabla ya kuwa golikipa alikuwa anacheza nafasi ya ushambuliaji lakini alivutiwa zaid na udakaji na golikipa wa yanga Yoberko wakati huo akiwa mchezaji wa yanga.

 Suleiman ambaye amewahi kuwa mshindi wa tuzo ya mashindano ya JK yaliyofanyika mwaka jana na kufanya kuibuka golikipa bora wa mashindano hayo,Bombom ilimfanya qweze kushiriki mashindano mbalimbali kama vile COPA coca cola,JK inasifika kuibua vipaji kama vile Ramadhani sigano kwa sasa anachezea Azam fc,Ibrahim ajibu anachezea timu ya yanga na Hassan isiaka anayekipaga timu ya mtibwa sugar.

 Akielezea mambo asiyoweza kuyasahau Suleimani alisema’’sitosahau  niliposhindwa kufuzu kucheza timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka kumi na saba 17[Serengeti boys];jambo lingine ambalo sitoweza kusahau niliposhindwa kucheza soka kwa kipindi cha miezi hisiyopungua miwili’’.hayo yamesemwa na Suleiman.


Timu aliyoifurahia katika maisha yake ya soka  ni Bombom Fc anayoitumikia mpaka sasa,vile ilimpaumaharufuna mafanikio alioyapata katika maisha yake ya soka;pia ametoa ushauli kwa wachezaji chipukizi ambao wamekata tama kwenye soka na kuwaomba wasikate tama na badala yake wafanye mazoezi ya kutosha  ili wafikie malengo yao kwenye soka.

IMG-20171016-WA0067

[PICHANI NI GOLIKIPA WA BOMBOM FC SULEIMAN BERKO {KATIKATI}AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE.PICHA NA MAKTABA].





Na;Saraphina Shanes
Screenshot_2017-09-26-14-39-03 
  


 Wananchi wa jiji la Daressalaam wameiomba serikali kutilia mkazo suala la usafi katika siku ya jumaamosi ambapo wananchi hao wameiomba serikali ihakikishe watu wote wanafanya usafi katika mazingira badala ya kujifungia ndani hadi mda wa saa nne unapofika ndio wanafanya shughuli zao jambo ambalo limeonekana lipo kinyume na Agizo la mkuu wa mkoa Mh.Paul Makonda linalowataka watu wote wa jiji hilo wafanye usafi
Wananchi wa jiji hilo wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na usafi,ambapo baadhi yao wamesema  kuweka mazingira safi  ni jukumu la kila mwanachi, wapo waliosema kuwa mda uliowekwa sio rafiki hivyo ni bora mda ukapunguzwa baada ya mwisho saa nne  iwe saa tatu kutokana na mda wa masaa mawili yaani saa kumi na mbili hadi saa mbili ni muda unaotosha kufanya usafi.
Katika mahojiano na baadhi ya wananchi mwandishi wetu alifanikiwa kuongea na mkazi wa Ilala jijini Daressalaam Ndugu Joseph .K. Christopher:”Alisema kuwa ni kweli wanajua suala hili ni zuri kwa jamii kulifuatilia na kuhakikisha kila mmoja anafanya usafi kwenye eneo aliopo ili kuepusha magojwa ya mlipuko kama kipindupindu na Kuhara.
Akiongeza ndugu Joseph .K. Christopher amesema serikali inalengo zuri na nchi yetu hasa jiji hili la Daressalaam amabalo watu wa nchi  mbalimbali wanalitembelea,Pia uwepo wa Wizara muhimu jambo ambalo linatakiwa kufanya jiji kuwa safi na kuendana na hadhi yajiji lenyewe kuwa la kimataifa.hayo yalisemwa na mkazi huyo.
Pia mwandishi wetu alipata  kuongea na mmoja wa wafanya biashara Ndugu Said Sanze ambae ameipongeza serikali pamoja na kusema kuwa ni sawa kabisa kutenga siku ya usafi na ikiwezekana ziongezwe siku na kufanya sikuzote ziwe za usafi na kuweka wasimamizi ambao watafuatilia kwa ukaribu  hili suala ili kuhakikisha kwa wale watakaoenda kinyue na sheria wanachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho ni maoni ya wananchi wa Daressalaam ambapo kwenye mahojiano na mwandishi wetu raia  wameishauri serikali iongeze nguvu kwenye suala hili kwa kutoa elimu kwa wananchi jinsi gani hii siku ilivyo na umuhimu na pia waelezewe kuhusu faida ya kuweka mazingira safi,Pia wamewaomba wananchi waishio jiji hilo kuachana na zana ya kuwa wanaotakiwa kufanya usafi ni wafanya biashara pekee badala yake watoe ushirikiano katika kuhakkisha jiji linakuwa safi.







Na;Neema Edson


image%2B%25281%2529
Mto Msimbazi umeacha njia yake na kujitengenezea njia nyingine katika eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam hali iliyosababisha baadhi ya nyumba kubomoka na kuhatarisha usalama wa nyumba nyingine pamoja na usalama wa wakazi wa maeneo hayo.
Katika eneo la JANGWANI, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM limelazimika kufunga barabara katika eneo hilo ili kunususru usalama wa watu na pia kulazimu huduma ya mabasi yaendayo haraka kusitisha safari zake.
Katika eneo la Jangwani Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limelazimika kufunga barabara eneo hilo ili kunusuru usalama wa watu na pia kulazimu huduma ya mabasi yaendayo haraka kusitisha safari zake.
PMTV imeshuhudia baadhi ya wakazi wa Jiji wakilazimika kuvuka katika eneo la Jangwani ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku. 
Eneo la Jangwani ni kati ya meneo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Mto Msimbazi unapita na kuleta madhara makubwa kwa wakazi wanaoishi karibu na mto huo, yakiwemo ya nyumba zao kujaa maji kipindi cha mvua.
Kwa ujumla mvua zilizonyesha kwa takriban siku mbili mfululizo hadi jana zimeleta adha kubwa katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam hali iliyomlazimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kufika eneo la Vingunguti na kutoa tahadhari kwa wakazi wa eneo hilo wanaoishi karibu na Mto Msimbazi.
Makonda amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.









Na;Neema Edson
20171017_173426%257E2

Wakazi wa yombo kilakala wilayani Temeke mkoani Dar es salaam wachoshwa na uchafunzi wa mazingira utokanao na viwanda katita mto yombo ambao husababisha uchafunzi wa mazingira pamoja na uchafunzi wa bahari ya hindi kwakua maji hayo hutiririka kuelekea baharini
.
Mmoja wa wakazi katika eneo hilo Bw. Seif Chekwa amezungumza na Umoja blog na kusema kuwa mto huo umekua ukichafuka kutokana na maji machafu yanayo toka viwandani kutiririshwa na kuelekezwa katika mkondo wa mto huo jambo ambolo huchafua mto huo na mazingira kwa ujumla.
Aidha Chekwa amesama maji hayo hutoa harufu mbaya ambo nikero kwa wakazi wanao zunguka mto huo jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wakazi hao pamoja na watoto wadogo wanacheza katika maji hayo machafu.

Mbali na hayo Chekwa  amedai kuwa kutokana na uchafuzi huo unasababisha ongezo la mbu katika eneo hilo ambao huambukiza ugonjwa wa maralia kwa kiasi kikubwa ingawaje watu wanajitahidi kujifunika vyandarua nyakati za usiku wanapo lala.

Vilevile mto huo awali  ulikua ukitumika katika shughuli mbalimbali zinazo wasaidia wakazi wa eneo hilo kama kuchota maji ya kutumia majumbani pamoja na shughuli za kilimo cha mbogamboga katika mashamba yaliyopo katika mbonde la mto huo hivyo shughuli hizo zimekatishwa kutokana na uchafuzi huo.

Pia Chekwa ameiomba serikali kuingilia kati suara hilo ili kukomesha tatizo hilo na kuhakikisha wamiliki wa viwanda wanatengeneza mfumo mzuri wa kuhifadhi maji hayo machafu ili kuunusuru mto huo pamoja na afya za wakazi hao

Kwa  picha zaidi zinozo onosha hali harisi ya mto Yombo.
20171017_173457%257E2


20171017_173508%257E2


20171017_173352%257E2


20171017_173339%257E2



20171017_173320%257E2














Screenshot_2017-11-04-20-10-11
Wananchi wa Yombo kilakala wilayani Temeke waitaka serikali kuongeza magari ya kuzelea taka , haya yameongelewa na wananch hao baada ya uchache wa magari hayo jambo linalo pelekea mrundikano wa takataka  na kusambaa katika makazi ya watu baada ya sehemu iliyo andaliwa kukusanyia taka kufurika wingi wa taka hizo.

Aidha mmoja wa  wananchi hao Bi. Sabrina Komba ameiambia plan media kuwa ukosefu wa magari hayo unasababisha uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubbwa  hususa ni katika kipindi hiki cha mvua nyingi ambapo maji hubeba taka hizo na kuzisambaza katika makazi ya watu na zingine huingia katika mto yombo ambapo husafirishwa moja kwa moja mpaka baharini.
Screenshot_2017-11-04-20-11-14
Vilevile Bi. Sabrina mesema afya za wakazi hao ziko hatarini kutokana na uchafu huo ambao  unaweza kusababisha magojwa ya mripuko na kupoteza maisha ya wakazi hao hususa ni watoto wadogo wanao cheza michezo yao katika maeneo hayo.

Kwa upande wa mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Juma Matari amekiri kuwepo kwa uchafu huo na kudai kuwa  magari yamekua ni changamoto kubwa sana hivyo wapo katika mchakato wa kulitokomeza tatizo hilo na hivi karibuni hali itakua swari na wananchi wataishi kwa amani na afya zao zikiwa njema.

Pia Matari amewata  wananchi hao kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha tatizo hilo lina tokomea kabisa ili wakazi waishi katika mazingira masafi na salama kwa afya za wakazi hao.

Hata hivyo suala la usafi wa mazingira limekua changamoto katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam hususa ni katika kipindi hiki cha mvua jambo ambalo linaleta wasiwasi kwa afya za wakazi waishio katika jiji la Dar ea salaam kwa ujumla.


Richa ya mkuu wa mkoa Mh. Paul Makonda kuteua siku ya jumamosi kuwa siku ya usafi katika maeneo yote ya jiji la Dar es salaam siku hiyo imekua haizingatiwi katika baadhi ya maeneo na ndio maana tunaona maeneo mengi yakiwa machafu sana hususa ni katika masoko kama; Buguruni,Tandika, Tandale n.k
Screenshot_2017-11-04-20-10-42