Na Jacqueline Benson
UGONJWA wa moyo ni miongoni mwa ugonjwa usio ambukiza ambao
huathiri moyo na mishipa.
Ugonjwa wa moyo ni tatizo sugu la kiafya linalohusisha
kuongezeka kwa mkandamizo wa msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu.
Ulaji wa vyakula jamii ya korosho na karanga angalau mara mbili
kwa wiki, unaelezwa kusaidia kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo
kwa asilimia 25.
Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Havard nchini
Marekani, unaonyesha ulaji wa mbegu jamii ya korosho na karanga kiasi cha
kiganja kimoja cha mkono mara mbili kwa wiki, ni kinga dhidi ya magonjwa hayo.
Utafiti huo ulifanywa dhidi ya watu 200,000 kwa kipindi cha miongo
miwili, ambapo ilibainika aina zote za vyakula vya jamii hiyo vinasaidia
kuimarisha afya ya moyo.
Licha ya kwamba vyakula hivyo vina kiwango kikubwa cha
nishati ya kuupa mwili nguvu (kalori), lakini hakuna uthibitisho wowote ya
kwamba vinachangia kuongeza uzito wa mwili.
Jamii hiyo ya vyakula, kila kimoja hubeba kalori 150 hadi 190,
mafuta gramu 10 hadi 17, protini gramu 3 hadi 6.
Utafiti huo pia unaonyesha ulaji wa vyakula jamii ya
karanga na korosho unapunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi.

0 comments:
Post a Comment