Na Gladness Mapesa
WAKANDARASI wa eneo la Ubungo Kibangu Jijini Dar es salaam
walalamika wafanyakazi wa eneo hilo
hususani maman’tilie kwa kuuza vyakula
katika mazingira yasio salama
Wakizungumza na UMOJA BLOG mmoja wa wakandarasi hao Maiko
Ally alisema kutokana na mvua za masika
zilizoanza kunyesha maeneo mbalimbali, wamekuwa wakipata chakula hicho katika
mazingira machafu jambo ambalo linaweza
kuleta mlipuko wa magonjwa hususani kwa gonjwa la kipindupindu katika eneo hilo
Ally alisema kuwa kutokana na hali hiyo wanawaomba
wafanyabiashara hao kuwauzia chakula hicho katika mazingita safi
“Sisi wakandarasi wa
eneo hili tunawaomba mamantilie wanaotupikia chakula katika eneo hili waboreshe mazingira ya kufanyia kazi zao za
uuzaji wa vyakula kwani mazingira ni machafu na hutupa wakati mgumu sisi walaji
na wengine hula wakiwa wamesimama ”alisema Ally
Mmoja wa wauzaji wa vyakula eneo hilo aliyejitambulisha kwa
jina la Imelida Peter anaandaa chakula katika sehemu safi na salama titizo ni kwa
wakandarasi wenyewe hutumia eneo hilo kwa haja ndogo pindi waendeleapo na kazi
zao.
“siuzi chakula katika mazingira machafu mimi naandaa chakula
change katika sehemu safi na salama titizo ni kwa wakandalasi wenyewe hokojoa
katika eneo hilo pindi waendeleapo na kazi zao na wengine kutoa hata haja kwa pembeni
ya eneo hilo kwani lipo kalibu na kichaka”
“ Mkandarasi mkuu ndio aliyeniomba mimi kuwapikia chakula
ili kuokoa muda wao kwenda mbali kufuata chakula”alisema Imelida
UMOJA BLOG lilizungumza
na Mkandarasi Mkuu wa eneo hilo yeye
alijitambulisha kwa jina moja la Thomas
ambapo alisema alikubali mazingira wanayotumia kwajili ya chakula
sio salama na yeye ndio alimuomba mama uyo awe anawapikia chakula
“ Kwaupande wa mazingira machafu tatizo lipo kwa wakandarasi
wenyewe sio maman’tilie huyo kwani wengi
hao wamekuwa wakitoa haja zao karibu na eneo hilo la kupatia chakula
UMOJA BLOG ilipojaribu
kumtafuta mwenyekiti wa eneo hilo ili kuweza kutolea ufafanuzi suala hilo
lakini hakuweza kupatikana

0 comments:
Post a Comment