Wednesday, 16 May 2018

ASILIMIA 17 YA WATOTO HUZALIWA NJITI



NA REGINA PETRO
Takwimu nchini zinaonesha kuwa asilimia 17 ya watoto huzaliwa kabla ya muda wa mimba kukomaa.taarifa hiyo inetolewa na Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu.


Waziri Ummy Mwalimu akiwa anaongea na wananchi.
Waziri Ummy alisema Wizara yake imekuwa na inaendelea kuchukua hatua mbalimbali huboresha huduma kwa watoto hao ili kuepusha vifo. Alisema watoto njiti huwa katika hatari zaidi ya kupoteza maisha kutokana na kutokomaa kwa mapafu,kupoteza joto la mwili kwa haraka zaidi, kupata mahabukizo ya bakteria, kushidwa kunyonya na kupata manjano.
Alisema ili kukabliana na tatizo hilo hatua mablimbali zimekuwa zikitekelewa.
Alizitaja hatua hizo kuwa ni kuwapatia wajawazito dawa ya kusaidaia mapafu ya mtoto kukomaa haraka, kuanzisha huduma za mama kangaruu katika ngazi ya hospitali, kununua na kusambaza vifaa vya kuhudumia watoto njiti wenye matatizo ya kiafya.
 

‟wizara inaendelea kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ya ngazi ya jamii, ili waweze kutoa elimu kwa wananchi kuhusa masuala mbalimbali ya afya ya uzazi na mtoto ikiwemo dalili za hatari wakati wa ujauzito,”alisema
Aidha alisema kwamba ni vyema wanawake wakahudhuria kliniki mapema ili waweze kutambuliwa matatizo yao na pia kupata elimu mbalimbali ikiwamo haja ya kuwa na mapumziko ya kutosha

0 comments:

Post a Comment