Na;Edward Benson
Msanii
chipukizi wa nyimbo za kumsifu mungu[injili]nchini Tanzani a anaefahamika kwa
majina ya Betha Mwafilombe,amevunja ukimya kwa kusema anajishughulisha na
kilimo cha mpunga lengo lake likiwa ni kujihimalisha kifedha ili kufikisha
muziki wake mbali.
Hayo
ameyasema alipokuwa akizungumza na Umoja blog katika mahojiano ya
hivi karibuni yaliyofanyika kwa njia ya simu.
Changamoto
kubwa anayo kutana nayo kwasasa ni ukosefu wa soko la kudumu la kuuzia kazi
zake zilizo kwenye mfumo wa CD ambapo jambo hilo limekuwa tatizo kutokana na
utandawazi wa watu kunyonya vitu mitandaoni kwa kutumia simu na
kiamba mpakato[computer].
Betha
anatarajia kufanya uzinduzi wa albam yake mpya inayo kwenda kwajina la kwa
Neema ndani ya mwaka huu mala baada ya kukamilisha taratibu zote na kutaja kuwa
utakua uzinduzi wa historia katika taifa la Tanzania.
Amemaliza
kwakuomba ushirikiano kutoka kwa mashabiki wa kazi zake kwa mchango wa pesa au
mawazo ili kuisogeza huduma yake kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

0 comments:
Post a Comment