Na Juliani Kasimiri
Mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa
Dar es salaam zimeonekana kuwa gumzo kubwa hii ni kutokana na mvua izo kunyesha
mara kwa mara,nakupelekea athari kubwa kwa wakazi wa mkoa huo hususani wa
maeneo ya mabondeni

Mvua hizo
zinatakribani wiki moja tokea zianze kunyesha katika maeneo mengi mkoa humu,lakini
zimeonekana kuwa na athari kubwa za kiuchumi na kimiundombinu.

Hussain
Bakari ni mfanyabiashara katika soko la buguruni,kwa upande wake mvua hizo
zimemfanya ashindwe kufanya biashara zake za kupanga mboga mboga hii ni
kutokana na kunyesha mara kwa mara kwa mvua hizo.

Asha Mussa
ni mkazi wa buguruni yeye anaona mvua hizo zimefanya usafiri kuwa mgumu hususani
anapotaka maeneo yake ya kazi kuelekea nyumbani.
Ata ivyo
watu mbali mbali katika mkoa huo wameonekana kuendelea na shughuli zao za
kujipatia kipato,licha ya mvua hizo kuendelea kunyesha katika maeneo mengi jiji
hapa.
0 comments:
Post a Comment