Wednesday, 16 May 2018

WATOTO OMBAOMBA KUWA KERO BARABARANI.

Na Saumu S. Mohammed.
   Wanajamii wa mtaa wa buguruni waonekana kukerwa na tabia ya watoto wanaokaa pembezoni mwa babara huku wakionekana kuombaomba wapita njia kwa mujibu wa kujikimu pamoja na wazazi wao.
watoto ombaomba barabarani
  Wazazi  wa watoto hao husemekeana kuwa  kando ya barabara huku wakiwatuma watoto wao kufanya zoezi hilo bila kujali kwamba wanaatharisha maisha yao kwa kuwatuma   barabarani kwani vyombo vya usafiri vinapita kwa kasi.

   Watoto hao ni wadogo sana kuelewa usalama wao,kwani wao hutimiza mujibu waliopewa na wazazi wao. Salma ni mmoja wa watoto hao ambae tulipata fursa ya kuzungumza nae na akasema yeye huamrishwa na mama yake kufanya hivyo ili aweze kupata chakula cha siku nzima.
"Mama anaponambia niombe pesa na yeye hukaa kando kwenye kivuli ili ninapopata pesa hizo nimpelekee aweze kupata ya matumizi na nsipofanya hivyo mara nyingi tunakaa bila chakula.”

                                                                                                                            [picha na sadick]

0 comments:

Post a Comment