Na;Saraphina Shanes
Wananchi wa jiji la Daressalaam wameiomba
serikali kutilia mkazo suala la usafi katika siku ya jumaamosi ambapo wananchi
hao wameiomba serikali ihakikishe watu wote wanafanya usafi katika mazingira
badala ya kujifungia ndani hadi mda wa saa nne unapofika ndio wanafanya
shughuli zao jambo ambalo limeonekana lipo kinyume na Agizo la mkuu wa mkoa
Mh.Paul Makonda linalowataka watu wote wa jiji hilo wafanye usafi
Wananchi
wa jiji hilo wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na usafi,ambapo baadhi yao
wamesema kuweka mazingira safi ni jukumu la kila mwanachi, wapo waliosema
kuwa mda uliowekwa sio rafiki hivyo ni bora mda ukapunguzwa baada ya mwisho saa
nne iwe saa tatu kutokana na mda wa
masaa mawili yaani saa kumi na mbili hadi saa mbili ni muda unaotosha kufanya
usafi.
Katika
mahojiano na baadhi ya wananchi mwandishi wetu alifanikiwa kuongea na mkazi wa
Ilala jijini Daressalaam Ndugu Joseph .K. Christopher:”Alisema kuwa ni kweli
wanajua suala hili ni zuri kwa jamii kulifuatilia na kuhakikisha kila mmoja
anafanya usafi kwenye eneo aliopo ili kuepusha magojwa ya mlipuko kama
kipindupindu na Kuhara.
Akiongeza
ndugu Joseph .K. Christopher amesema serikali inalengo zuri na nchi yetu hasa
jiji hili la Daressalaam amabalo watu wa nchi
mbalimbali wanalitembelea,Pia uwepo wa Wizara muhimu jambo ambalo
linatakiwa kufanya jiji kuwa safi na kuendana na hadhi yajiji lenyewe kuwa la
kimataifa.hayo yalisemwa na mkazi huyo.
Pia
mwandishi wetu alipata kuongea na mmoja
wa wafanya biashara Ndugu Said Sanze ambae ameipongeza serikali pamoja na
kusema kuwa ni sawa kabisa kutenga siku ya usafi na ikiwezekana ziongezwe siku
na kufanya sikuzote ziwe za usafi na kuweka wasimamizi ambao watafuatilia kwa
ukaribu hili suala ili kuhakikisha kwa
wale watakaoenda kinyue na sheria wanachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho
ni maoni ya wananchi wa Daressalaam ambapo kwenye mahojiano na mwandishi wetu
raia wameishauri serikali iongeze nguvu
kwenye suala hili kwa kutoa elimu kwa wananchi jinsi gani hii siku ilivyo na
umuhimu na pia waelezewe kuhusu faida ya kuweka mazingira safi,Pia wamewaomba
wananchi waishio jiji hilo kuachana na zana ya kuwa wanaotakiwa kufanya usafi
ni wafanya biashara pekee badala yake watoe ushirikiano katika kuhakkisha jiji
linakuwa safi.

0 comments:
Post a Comment