CHANGAMOTO
za maisha ni njia ya mafanikio kwa binaadamu hivyo ndivyo ilivyo na hakuna
anaepingana na huu ukweli ambao umedhihirishwa na kijana wa kitanzania Bwana
Omari Hafidhi ambae amepitia mengi katika safari yake ya maisha,ambae
anahistoria ya pekee baada ya kupanga vyumba takribani 15 kwa nyakati tofauti
lakini sasa ni moja ya vijana walio na msaada mkubwa kwa vijana wengine.
Omari
Hafidhi ni mzaliwa wa Pemba kaskazini,amezaliwa mwaka 1980 katika
Hospitali ya wete,ambapo katika upande wa mama yake yeye ni motto wa 6 na
upande wa Baba ni mtoto wa 5,katika familia yao alikuwa akilelewa na mama
pekee,ambapo Omari alianza kujihusisha na shughuli ndogndogo za kujipatia
kipato akiwa na umri wa miaka kumi na mbili[12]ili kuisaidia familia.
Alipofikisha
umri wa miaka kumi na tano[15]alienda mjini Unguja ambapo alikuwa akijihusisha
na kazi ya uvuvi kwa mda wa miaka isiyopungua sita,na baada ya hapo alienda
jiji la Daresalaam mwaka 2000 ambapo alikuwa akifanya biashara ya kuuza matunda
akiwa kama mchuuzaji,alifanya biashara hiyo kwa mda wa mwaka mmoja na hatimae
alirejea tena Pemba.
Alipokuwa
pemba alipatwa na tatizo la kupigwa na lisasi ya mguu baada ya vuguvugu la
maandamano ya kisiasa yaliyotokea 2001ambapo alisaidiwa na wasamalia wema
na kumpeleka hospitali ya Mnazi mmoja iliyopo Zanzibar na bnaadae alihamishiwa
Daresalaam kwa matibabu zaidi katika hospitali ya Muhimbili,baaada ya hali ya
kiafya kuimalika omari aliruhusiwa kutoka hospitali hapop.
Aliporuhusiwa
alikuwa akiishi na mjomba wake Temeke ambapo al;ikuwa akifanya biashara ya
kuuza juisi katika mgahawa wa mjomba wake,na baadae alihamia bugurni ambapo
alipata kufungua mgahawa wake wa kuuzia juisi baada ya kupewa pesa na kiongozi
mmoja wa chama wa kisiasa alipokuwa anahitaji nauli ya kiasi cha fedha
tasiliumu za kitanzania shilingi 150,000 ili arudi kwao lakini akaona kama
fursa na baadae aliitumia pesa kuanzishia biashara yake ya juisi.
Omari
alifanikiwa kuiendeleza biashara yake ya juisi na haimae alifanikiwa kuwaajili
vijana wa kazi wasiopungua 26,ambapo aliongeza vitu v1ya biashara na alikuwa
akiuza vyakula mbalimbali pamoja na vinywaji ambapo alikuwa amefungua Café
iliyomuinua zaidi kimaisha na hatimae alifanikiwa kununua gari mbili za abiria
aina ya Costa,viwanja viwili chin na vingine Pemba,pia amefanikiwa kujenga
nyuma mbili ambapo zilizopo buguruni ambazo zina thamani kubwa.
Pia
omari amefanikiwa kumlea mtoto wa kaka yake aliefariki 2006,kwa sasa
amefanikiwakumlea mtoto huyo ambaye kwa sasa yupo kidato cha sita,pia omari ana
watoto watano[5]ambao anaishi nao,pia hadi sasa amekuwa akiendelea na biashara
yake ya juisi ambayo imekuwa ni chachu kwenye mafanikio yake,
0 comments:
Post a Comment