Na;Neema
Edson
Mto Msimbazi umeacha njia yake na kujitengenezea njia nyingine
katika eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam hali iliyosababisha baadhi ya
nyumba kubomoka na kuhatarisha usalama wa nyumba nyingine pamoja na usalama wa
wakazi wa maeneo hayo.
Katika eneo la JANGWANI, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM
limelazimika kufunga barabara katika eneo hilo ili kunususru usalama wa watu na
pia kulazimu huduma ya mabasi yaendayo haraka kusitisha safari zake.
Katika eneo la Jangwani Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam limelazimika kufunga barabara eneo hilo ili kunusuru usalama wa watu na
pia kulazimu huduma ya mabasi yaendayo haraka kusitisha safari zake.
PMTV imeshuhudia baadhi ya wakazi wa Jiji wakilazimika kuvuka
katika eneo la Jangwani ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila
siku.
Eneo la Jangwani ni kati ya meneo ya jiji la Dar es Salaam
ambapo Mto Msimbazi unapita na kuleta madhara makubwa kwa wakazi wanaoishi
karibu na mto huo, yakiwemo ya nyumba zao kujaa maji kipindi cha mvua.
Kwa ujumla mvua zilizonyesha kwa takriban siku mbili mfululizo
hadi jana zimeleta adha kubwa katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam
hali iliyomlazimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kufika eneo la
Vingunguti na kutoa tahadhari kwa wakazi wa eneo hilo wanaoishi karibu na Mto
Msimbazi.
Makonda amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchukua tahadhari
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

0 comments:
Post a Comment