NA REGINA
PETRO
Waziri wa
afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema upimaji
wa kifua kikuu(TB) na ukimwi kwenye baa hautakuwa wa lazima .
Waziri Ummy
Walimu waliutumia wananchi.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho wa miaka 30 ya mpango wa Taifa wa kudhibiti ukimwi
(NACP), Mwalimu alisema baada ya kutolewa taarifa ya kuwepo mpango huo watu
wengi wamekuwa na hofu. ‟Tutatekeleza mpango wa kusogeza huduma za upimaji TB
na ukimwi kwenye naa, ila hautakuwa wa lazima, tuachofanya ni kuwashawishi
wananchi kutumia fursa ya kusogezewa huduma hiyo,’’
Upimaji kwa
hiari wa mtu mmoja mmoja .
Aidha,
alisema kwa sasa wizara yake iko kaktika mkakati wa kufanyaia marekebisho ya
sharia ya Ukimwi kwa lengo la kuruhusu watu kujipima mwenyewe, kutoa fursa kwa
vijana kuanzia miaka 15kwenda kupima ukimwi bila kupata ridhaa ya wazazi ay
walezi.
Katika hatua
nyingine,Mwalimu aliagiza kuanzia Julai mosi mwaka huu, watu wanaoishi na
virusi vya ukimwi kupewa dawa za miezi mitatu badala ya sasa ya kupewa kwa
miezi mwili. Agizo alilitoa kutokana na Mwenyekiti wa baraza la watu kudai kuwa
utaratibu wa kupewa dawa za miezi miwili umekuwa ukiongezea gharama,kwani
wamekuwa wakitakiwa kupima afya zao kila baada ya miezi mitatu. Waziri huyo
alisema utaraibu huo wa kuwapa dawa miezi mitatu mitatu uanza haraka isipokuwa
kwa wale ambao wanaonekana hawataweza kutuza dawa hizo au ambao ndio kwanza
wanaznza kutumia dawa hizo.



0 comments:
Post a Comment