Wednesday, 16 May 2018

WAATHIRIKA WA KISUKARI WAONGEZEKA DUNIANI.




Na Jacqueline Benson
KISUKARI aina ya ugonjwa unaoendelea kutajwa  kusumbua watu wengi hususan wenye kipato cha juu. Sababu za ugonjwa huo zinaelezwa na wataalamu lakini zimekuwa zikipuuzwa huku wanaosema ugonjwa huo  ni wa watu wenye kipato cha juu wakizidi kuangamia pasi na kujua.
Hiyo inaifanya idadi ya watu wanaopoteza maisha kuongezeka ambapo kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kwa mwaka 2005 kati ya vifo milioni 58 vilivyotokea watu miilioni 35 walifariki kwa magonjwa yasiyoambukiza na huku magonjwa hayo yakizidi  kuongezeka hasa hapa nchini .




Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa NIMRI kwa mwaka 2012 ilitoa ripoti ya ongezeko la visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza. Utafiti huo unaonyesha uvutaji wa sigara unachangia magonjwa yasiyoambukiza kwa asilimia 15.9 unywaji pombe kwa asilimia 29 wanaotumia matunda na mbogamboga mara tano kwa wiki asilimia 97 wanene kupitiliza asilimia 26 wanaotumia mafuta mengi asilimia 35 na shinikizo la damu asilimia 25.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2015 inakadiriwa watu milioni 1.6 wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari. Daktari Bingwa Matibabu Ugonjwa wa kisukari na Homoni Banduka Elisante alisema ugonjwa wa kisukari  unatokana na kuongezeka kwa  kiwango cha sukari katika damu na kusababisha mfumo wa unaodhibiti sukari mwilini kushindwa kufanya kazi
 

0 comments:

Post a Comment