Friday, 18 May 2018

MAKONDA ATOA ONYO KALI KWA WANAWAKE

Na Shani Seif

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaonya wasichana wa mkoa wake wa Dar es salaam kutokubali kuolewa na wanaume wanaoishi katika maeneo ya bondeni ambayo ni hatarishi hasa katika kipindi cha mvua za masika.



Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam


Makonda amesema hayo alipofanya ziara katika eneo la mbagala kiburugwa na kuona baadhi ya nyumba za wananchi ambazo zimeathirika kutokana na kujengwa katika maeneo hatarishi na kuwataka wakazi hao kuhama mara moja.

Makonda ameongeza kuwa serikali  haitaweza kutoa msaada wa chakula na malazi kila mara kwa wananchi ambao wanakumbwa na majanga yanayotokana na wao kuamua kukaa katika maeneo hatarishi kwa kujitakia.




Baadhi ya wakazi wanaokaa mabondeni

Mkuu wa mkoa huyo amedai kuwa maeneo hayo ni ngumu kwa mwananchi kupata msaada wa dharura ikiwemo gari la wagonjwa au huduma ya zima moto.

0 comments:

Post a Comment