Wednesday, 16 May 2018

MAANDALIZI YA MTIHANI.

Na Saumu S. Mohemmed.
Zikiwa zimesalia wiki mbili tu kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari, TIME SCHOOL OF JOURNALISM  kufanya mitihani yao wa mwisho wa muhula . Wanafunzi wameonekana kujituma kwa jitiihada zao zote pamoja na kukamilisha kazi za walimu.
Akiongea nasi  Asha John mmoja ya wanafunzi chuoni hapo amesema kuwa, amefurahishwa sana na kitendo cha walimu kuongeza siku mbele za kufanya mtihani wao, kwani ndioo wamepata nafansi nzuri yakuweza kujiandaa kwa ufasaha kabisa.
 “Kwa upande wangu mimi nimefurahishwa sana na kitendo walichokifanya walimu wetu kutuongezea mda tuzidi kujiandaa na mtihani utakaoanzaa tarehee 28 mwezi huu. Mana ukiangalia baadhi yetu tulikua hatujakamilisha ada hivyo tusingeweza kufanya mtihani huo.

maandalizi ya mitihani
Hata hivyo mwalimu mkuu wa chuo hicho Bi. Blandina Semaganga amewasii wanafunzi wake kujiepusha na kesi za kuibia mtihani pindi siku zikiwadia  na pia kuwatakia mtihani mwema wanafunzi wote. 

0 comments:

Post a Comment