Na. Maua Patrick.
Kiwanda cha uzalishaji wa
saruji cha kampuni ya Dangote kimetoa mifuko 2400 ya saruji kwa mkuu wa mkoa wa
mtwara kwa ajili ya ujenzi wa maendeleo ya madarasa , vyoo pamoja na nyumba za
walimu kwa shule za halmashauri ya manispaa Mtwara.
Amezungumza na CHIPUKIZI Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Mtwara FRANSICS TRIPHONY MKUTI ameeleza kuwa mifuko ya saruji kutoka kwa Mwezeshaji Dangote itakidhi mahitaji na kuwezesha ujenzi huo kwa asilimia kubwa.
“Tunaomba wawezeshaji wengine
wajitokeze ili tuweze kuendesha hili suala la utengenezaji wa madarasa na vyoo
vya kila shule wilayani Mtwara kwa wepesi zaidi. hakika mifuko tuliyopokea
kutoka kwa Dangote itakidhi mahitaji kwa asilimia kubwa katika ujenzi na kubaki
na vitu vidogo vidogo” Alisema Mkuti
Pia FUNDIKILA MASAMALO akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara amesema kuwa anahaidi kutumia mifuko ya saruji hiyo na kukamilisha ujenzi ipasavyo ili watoto wapate kusoma kwa usalama zaidi kwa mazingira safi na ulinzi wa afya zao.


0 comments:
Post a Comment