Na;Neema Edson
Wakazi
na watumiaji wa barabara inayo unganisha Buguruni kwa mnyani na Vingunguti
machinjioni jijini Dar es salaam wapaza sauti zao baada ya kukutana na kamera
ya Plan Media wakilalamikia ubovu wa barabara hiyo na kuiomba serikali
kuiboresha barabara hiyo ambayo imegubikwa na ubovu kwa muda mrefu pasipo
kuikarabati.
Aidha
barabara hioyo ina mashimo mengi pamoja na kujaa maji katika mashimo hayo
kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha jambo ambalo linasababisha wananchi
hao kuitumioa kwa taabu na kusababisha foreni ya magari amboyo huwasababishia
watu kuchelewa katika safari zao.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao walikua na haya yakusema, Bw.
Shaaban Songo ambae ni kondakta wa gari la abiria linalo fanya safari zake kati
ya Vingunguti na Mnazimmoja amesema barabara hiyo imekua kero sana ambapo
husababisha magari yao kuharibika marakwamara kutokana na mashimo ya barabara
hiyo.
Vilevile
Bi. Maryam Marwa ambae ni mkazi wa Vingungunti dereva wa gari binafsi
amesema wanalazimika kubuni njia za vichochoroni wakihofia kuharibika kwa
magari yao huku wakiingia garama kubwa ya mafuta pamoja na muda kwasababu
huwapasa kutembea taratibu sana.
Kwa
upande wa Bw.Hasheem Mhina ambae pia ni mkazi na mfanya biashara wa
vingunguti amesema wanapata shida kupitisha mizigo yao kwa kutumia magari
makubwa ya mizigo wakihofia kuzama kwa magari hayo kwasababu ubovu huo unatisha
mno.
Pia
Bw. Husien Mpilaru ambae ni serikali ya mtaa amesema anafahamu ubovu wa
barabara hiyo na kuiambia plan media kwamba babara hiyo haiko chini ya manispaa
ya ilala bali ipo chini ya TAKULA ambao walitakiwa waitengeneze tarehe
5/10/2017 huku mpaka leo hakuna dalili za TAKULA kuitengeneza barabara hiyo.
Vilevile
Mpilaru ameongeza na kusema kuwa anaiomba serikali kuja kuiangalia barabara hii
na kuifanyia ufumbuzi ili kuiondoa kero hii ya muda mrefu ili wakazi hao
waitumie kwa amani katika shughuli zao mbalimbali ikiwemo usafirishaji katika
kujenga taifa.




0 comments:
Post a Comment