Na Juliani Salvatory.
Kuongezeka kwa mashimo katika Bara bara
nyingi mkoani Dar es salaam kumeonekana kuwa ni kelo kubwa kwa madeleva
watumiao bara bara hizo.

Licha ya
Serikali kutumia gharama kubwa katika utengenezaji na ukarabati wa miundombinu
hiyo ya bara bara,lakini bara bara hizo zimeonekana kuwa chini ya kiwango
kinachopelekea kuwa na mashimo mengi katika jiji la Dar es salaam.

Sadam
Jumanne ni dereva boda boda maeneo ya buguruni,kwa upande wake anaona mashimo
hayo yamezidi kuwa mengi na kuiomba
serikali kuchukuwa hatua katika kukarabati miundombinu ya bara bara hizo.
Bakari Simi
yeye ni dereva wa dala dala ziendazo Buguruni-Makumbusho,kwa upande wake
anaiomba serikali kuchukua juhudi za haraka katika kukarabati mashimo hayo
kwani upelekea ubovu wa vyombo vyao vya usafiri.

Wakandarasi
wanaopewa tenda ya kutengeneza miundombinu ya bara bara wanapaswa kutengeza
bara bara zenye ubora na zinazokidhi maitaji ya watumiaji wa bara bara
hizo,kwani itasaidia kuepusha ajali mbali mbali zisizo na hulazima.
0 comments:
Post a Comment