Wednesday, 16 May 2018

Na;Saraphina Shanes

Wakazi wa buguruni mkoani Dar es salaam walalamikia ongezeko la ada ya uzoaji wa taka kutoka shilingi elfu tano (5000) hadi shilingi elfu saba (7000) katika hali isiyo ya kawaida wakazi hao walalamikia serikali ya mtaa huo kwa ongezeka hilo la shilingi elfu mbili (2000).

Wakati wa mahojiano na mwandishi wetu wakazi hao wameiambia umoja blog kuwa mbali na ongezeko la ada hiyo wamekua wakicheleweshewa gari za kubebea
Screenshot_2017-08-24-22-24-24 takataka ambapo inapelekea kuwepo kwa mrundikano wa takataka  ambazo husababisha madhara kiafya
Umoja blog ilimtafuta mwenyekiti wa mtaa Ndugu.Karim Marapa alisema kuwa nikweli ada imepanda katika uzoaji taka ikiwa ni makubaliano ya serikali ya mtaa pamoja na wananchi wake.
Aliendelea kuzungumza ndugu Marapa kuwa wananchi wananchi wanatakiwa kuwa na uvumilivu na serikali yao kwani kero zao zinafanyiwa kazi hivyo ni vizuri wakatoa ushirikiano ili kuisaidia serikali kuwatimizia yale waliyo waahidi.

Mwisho kabisa ni maoni ya mwananchi ambapo mwandishi wetu alipata kuzungumza na Ndugu.Beshe Buhira ambae ni mkazi wa mtaa huo alisema kuwa anawaomba wahusika wa ukusanyaji wa takataka katika mtaa huo waongeze bidii katika kazi yao ili kuhakikisha wanajenga uhusiano mzuri na wananchi.

0 comments:

Post a Comment