Wednesday, 16 May 2018

WAKAZI WA BUGURUNI MATATANI KUKUBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO


Na,Gladness Mapesa

Wakazi wa Bugurini mtaa wa kisiwani wameilalamikia serikali kutolekebisha miundombinu ya kupitisha majitakanasehemu yakuhifadhia uchafu kwaajili ya matumizi ya nyumbani


Wakizungumza wakazi hao katika mkutano wao wakila mwezi unaofanyika kwa mwenyekiti wao wa mtaa bwana Masudy Ally walimlalamikia kiongozi huyo kwa kuchelewa kutoa uchafu majumbani mwao

Akizungumza na UMOJA BLOG mmoja wa wakazi hao yeye ni mfanyabiashara ya kuuza vitafunwa Bi Mariamu alisema swala lakuchelewa kuchkuliwa kwa uchafu limekuwa nikero kwa wakazi wa eneo hilo

“ Ukweli ni kwamba huo unachukua mu  alisema Bi Mariam
da mrefu sana hadikuja kubebwa hivyo huleta harufu mbaya katika banda lake jambo ambalo linasababisha kupoteza baadhi ya wateja wangu kwa kuhofia magonjwa ya mlipuko”

Pia akizungumza mkazi mwingine ambae hakutaka kutajajina lake aliongeza kuwa  tatizo linguine nikuto funukwa kwa mtaro uliopita karibu na nyumba yake hivyo umekuwa ukimpa wakati mgumu kwa motto wake wa miaka miwili amekuwa akitumbukia kwenye mtaro huo kwaajili ya kuchezea maji nakuokota makopo  yanayopita katika mtaro huo
Amesema haliiyo inampelekea wasiwasi  kwa maisha ya motto wake asije akapoteza maisha kwakukosa uangalifu endapo hatokuwa nyumbani

Wakati huohuo mwenyekiti Bwana Masudy Ally  Alisema changamoto inayo wakabili ni kuchelewa kutoapesa kwaajilin ya kubebewa uchafu na wengine kugoma nakutokulipa pesa izo Mwenyekiti huyo yeye alizitupia lawama ngazi ya manispaa kwa ujumla ambapo alisema wao ndio wenye dhaman ya kisimamia swala zima la miundombinu ya mtaa kwani wao ndio hukusanya pesa kwa wananchi kwaajili yakufanya marekebisho kwaajili ya miundombinu

Hivyo mwenyekiti pamoja na wakazi wa Buguruni kisiwani kwa ujumla wameitaka serikali kutimiza ahadi yao walio waahidi  wakati wa  uchaguzi kwani miundombinu hiyo inawapa shida na kuwafanya wananchi we ngine waugue magonjwa ya mlipuko na kuwapelekea hofu ya kupata magongwa ya  mlipuko kwa mazingira machafu yanao wazunguka.


0 comments:

Post a Comment